Mechi nne zimechezwa wiki hii, wababe wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) wakizichanga karata zao kwenye madimba tofauti kwenye raundi ya 11.Mechi hizo zikiendelea kwa raundi hiyo, zilifunguliwa na Simba Queens Januari 26, 2026 akikipiga dhidi ya Geita Queens kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza na kumalizika kwa Simba Queens kupata ushindi wa mabao 4-0.Hata hivyo, raundi hiyo imeendelea Januari 28, 2026 kwa michezo mingine mitatu, Yanga Princess ikiwa ugenini imefanikiwa kubeba pointi zote tatu mbele ya Bunda Queens kwa ushindi wa mabao 3-1.Mchezo mwingine ni ule uliopigwa Dar es Salaam. Tausi FC ikijazia kibaba chake cha pointi baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ceasiaa Queens, mchezo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.Suluhu kati ya Ruangwa Queens na Fountain Gate Princess iliyopigwa Uwanja wa Majaliwa, Lindi ndio iliyofunga hesabu za Januari 28.Mechi zilizosalia kukamilisha raundi hiyo ni Mashujaa Queens dhidi ya Bilo FC, na JKT Queens dhidi ya Alliance Queens.

    Share.