Timu ya taifa ya wanawake chini ya miaka 17 (Serengeti Girls) imepata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tunisia katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Machi 29, 2026 kwenye Uwanja wa Mustapha Ben Jannet mjini Monastir.

    Serengeti Girls ilitawala vipindi vyote vya mechi hiyo na kufanikiwa kufunga bao kipindi cha kwanza, na mengine mawili kipindi cha pili.

    Mfungaji wa bao la kuongoza alikuwa Yasinta Michael dakika ya 17, kabla ya Bahati Steven kupachika pili dakika ya 53, wakati Harrier Juma akifunga la tatu dakika ya 90.

    Akizungumza baada ya mechi, Kocha Mkuu wa Serengeti Girls, Bakari Shime alisema:

    “Mechi ilikuwa nzuri na wapinzani wetu wameonesha ushindani mkubwa. Nimefurahishwa na kiwango ambacho wachezaji wangu wamekionesha , nina imani watafanya vizuri zaidi mchezo unaofuata.”

    Serengeti Girls itacheza mechi ya marudiano na Tunisia tarehe 4 Aprili 2026 Uwanja wa Mustapha Ben Jannet, Monastir.

    Share.