Nne zafuzu nusu fainali RCL

    Timu nne zimefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) 2026 inayofanyika mjini Kigoma.

    Kajuna (Kigoma), Stand FC Masasi (Mtwara), Madini Kahama (Shinyanga), na Mount Hanang (Manyara) ndizo zitakazocheza hatua hiyo baada ya kushika nafasi mbili za juu katika makundi yao.

    Mechi zote za nusu fainali zitafanyika tarehe 30 Aprili katika Uwanja wa Lake Tanganyika.

    Madini Kahama na Stand FC Masasi zitacheza nusu fainali ya kwanza kuanzia saa 8 kamili mchana. Nusu fainali ya pili kati ya wenyeji Kajuna FC na Mount Hanang itaanza saa 10.30 jioni.

    Mechi ya fainali na ile ya kutafuta mshindi wa tatu zitafanyika tarehe 2 Mei kwenye uwanja huo huo.

    Share.